Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapalestina ungananeni kwa misingi ya PLO- Guterres

Wapalestina ungananeni kwa misingi ya PLO- Guterres

Katika siku ya mwisho ya ziara yake huko Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesihi kuwepo kwa umoja kati ya wapalestina wa eneo hilo la Gaza na wale wa Ramallah. Patrick Newman na ripoti kamili.

(Taarifa ya Patrick)

Leo Jumatano, Bwana Guterres ametembelea makumbusho ya wayahudi ya Kibbutz Nahal Oz na hatimaye alikwenda ukanda wa Gaza na kutembelea shule  inayosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la usaidizi kwa wapalestina, UNRWA.

Bwana Guterres amesema..

(Sauti ya Guterres)

“Natoa wito wa Umoja. Jana nilikuwa Ramallah na leo niko Gaza, pande zote hizi ni sehemu ya Palestina moja. Hivyo nasihi muwe na umoja kwa mujibu wa misingi ya chama cha ukombozi cha Palestina, PLO. Mgawanyiko huu unakandamiza kusudio na harakati za wapalestina.”

Halikadhalika Katibu Mkuu amesema ana ndoto ya kuona eneo hilo takatifu Mashariki ya Kati likiwa na mataifa mawili ambayo ni Palestina na Israel, akisema suluhu ya mzozo ni maelewano ambayo yatatua pia janga la kibinadamu.

Bwana Guterres ametumia fursa hiyo pia kutangaza msaada dola milioni nne kutoka mfuko wa dharura wa usaidizi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, CERF ili kufanikisha operesheni za usaidizi Gaza.