Watu wa Asili kushirikishwa katika utekeleshwaji wa SDGs: Laitaika Sehemu ya 2

29 Agosti 2017

Mwaka huu ni miaka kumi tangu kupitishwa kwa azimio la kihistoria kwenye Umoja wa mataifa kuhusu haki za watu wa asili. Tangu wakati huo kuna hatua kubwa zimepigwa hususani barani Afrika has kuwatambua watu wa asili lakini pia kufahamu kuhusu azimio hilo la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo bado kuna changamoto nyingi hasa katika utekelezaji wa baadhi ya haki hizo zinazojumuisha , afya, elimu, ajira , sheria na nyinginezo. Katika Sehemu ya pili ya mahojiano yafuatayo, Flora Nducha wa idhaa hii amezungumza na Dr elfuraha Laitaika kutoka Tanzania ambaye ni mtaalamu huru wa jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa asili

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter