Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila uchao migogoro yaongezeka, mkakati wa uzuiaji ndio suluhu- O’Brien

Kila uchao migogoro yaongezeka, mkakati wa uzuiaji ndio suluhu- O’Brien

Mratibu wa Umoja Mataifa katika masuala ya usaidizi wa kibinadamu Stephen O’Brien, amesema licha ya juhudi za usaidizi wa kibinadamu, pengo la uhitaji limeongezeka hivyo jumuya ya kimataifa ina wajibu mkubwa wa kuongeza usaidizi.

O’Brien ambaye amengoza ofisi hiyo kuanzia kwa takribani miaka mwili na nusu, amefanya mahojiano maaluma na redio ya Umoja wa Mataifa  na kusema licha ya kazi hiyo kumuwia ngumu kilichomtia moyo kwa watoa usaidizi wa kibinadamu ni.

( Sauti O’Brien)

‘‘Ujasiri, uvumilivu na shauku ya watu hawa ambao wanataka kuhakikisha watu walioathiriwa na migogoro, watu ambao hawana makosa, wanapata uokozi na ulinzi wanohitaji.’’

image
Mratibu wa Umoja Mataifa katika masuala ya usaidizi wa kibinadamu Stephen O’Brien anazungumza na mwanamke katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Dayniile Mogadishu, Somalia. Picha: UM/Tobin Jones
Akizungumiza namna ambavyo migogoro imeghubika dunia na hatua za usaidizi, Mkuu huyo wa operesheni za kiutu amesema.

( Sauti O’Brien)

‘‘Tuko katika katika nafasi nzuri ya kusaidia mateso ya watu pale dharura zitokeapo.  Sasa tunahitaji kuendelea kujizatiti kufanya kazi nzuri, kuzuia migogoro na kuondoa mateso ya watu.’’

Mteule huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  amezungumzia pia mabadiliko ya kimfumo na kiutendaji ya chombo hicho, kama ambavyo yaliwasilishwa na kiongozi huyo hivi karibuni akisema msisitizo wa Katibu Mkuu kuhusu uzuiaji wa migogoro kuwa msingi wa sera na uwezo wa Umoja wa Mataifa katika dunia tunayokabiliana nayo leo, na kutizama mbele hususani kwa idadi kubwa ya vizazi vya vijana kunahaja ya kuhakikisha inabadilishwa na kuakisi dunia hiyo.

Bwana O’Brien akaenda mbali zaidi na kusema sera hiyo inahitaji suluhisho zaidi la migogoro, kuzuia awali, ushirikiano mkuu wa wadau, utambuzi  wa matatizo ya dunia hususani ya kibinadamu, lakini pia kuwezesha maendeleo na usawa kwa haki za wanawake. Akiongeza kwamba yote hayo yanahitaji kuja pamoja katika namna ya kufaa kizazi cha leo.’’

Kuhusu mrithi wa nafasi ya Mkuu wa operesheni za usaidizi wa kibinadamu katika Umoja wa Mataifa , O’Brien ameshauri.

( Sauti O’Brien)

Kubwa zaidi, kutoka nje na kukutana na watu ambao tunawajibika kwao, watu ambao wanatuhitaji sana.