Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna hatua, lakini safari ni ndefu kutimiza haki za watu wa asili: Laitaika Sehemu ya 1

Kuna hatua, lakini safari ni ndefu kutimiza haki za watu wa asili: Laitaika Sehemu ya 1

Mwaka huu ni miaka kumi tangu kupitishwa kwa azimio la kihistoria kwenye Umoja wa mataifa kuhusu haki za watu wa asili. Tangu wakati huo kuna hatua kubwa zimepigwa hususani barani Afrika has kuwatambua watu wa asili lakini pia kufahamu kuhusu azimio hilo la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo bado kuna changamoto nyingi hasa katika utekelezaji wa baadhi ya haki hizo zinazojumuisha , afya, elimu, ajira , sheria na nyinginezo. Katika Sehemu ya kwanza ya mahojiano yafuatayo, Flora Nducha wa idhaa hii amezungumza na Dr elfuraha Laitaika kutoka Tanzania ambaye ni mtaalamu huru wa jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa asili