Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mashambulizi ya jimbo la Rakhine, Myanmar Kaskazini

UM walaani mashambulizi ya jimbo la Rakhine, Myanmar Kaskazini

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa huko Myanmar Bi. Renata Lok-Dessallien  amelaani vikali mashambulizi dhidi ya majeshi ya usalama katika Jimbo la Rakhine Myanmar kaskazini mapema Agosti 25.

Bi Dessallien ameelezea kusikitishwa na kupoteza kwa maisha ya wananchi huku akituma salamu za rambirambi  kwa familia zote na kuwatakia heri   katika kipindi hiki kigumu

Amezisihi pande zote kusitisha mapigano, ili kuokoa maisha ya wananchi, na pia kurudi katika mazungumzo ya kusaka amani.

Ameongeza kuwa matukio ya misiba  yanathibitisha umuhimu wa serikali kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Ushauri katika Jimbo la Rakhine kwa ajili ya kuboresha jamii zote.

Bi Dessallien amesema Umoja wa Mataifa una wasiwasi mkubwa  kuhusu hali ya usalama katika Jimbo la Rakhine na kwamba wanaendelea kufuatilia hali hiyo kwa kuwasiliana na mamlaka. husika