Skip to main content

Chuki dhidi ya jamii ya Igbo ni uchochezi wa machafuko: UM

Chuki dhidi ya jamii ya Igbo ni uchochezi wa machafuko: UM

Umoja wa Mataifa umelezea kusikitishwa kwake na vitisho na hatua ya kutakiwa kuondoka kwa watu wa kabila la Igbo huko Kaskazini mwa Nigeria, ifikapo Oktoba mosi mwaka huu. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Watalaamu wa Umoja wa Mataifa wamesema kwamba  vitisho dhidi ya kabila la Igbo vimekwenda mbali zaidi ambapo vimeambatana na wimbo wa chuki na ujumbe wa sauti kwa lugha ya Hausa , ukiwataka watu wa Kaskazini mwa Nigeria kuangamiza mali za watu hao na kumuua yeyote atakayekiuka agizo ifikapo Oktoba mosi.

Mmoja wa wataalamu hao ni Mutuma Ruteere anayengazia mifumo ya kisasa ya ubaguzi, ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na hali zingine za kutovumiliana.

( Sauti Mutuma)

Mtaalamu huyo amesema kwa kuwa mivutano hiyo ya kikabila ni ya kihistoria nchini humo.

( Sauti Mutuma)

Marufuku dhidi ya kabila la Igbo ambalo asili yake ni kusini mwa Nigeria, ilitolewa mnamo Juni 6, 2017 wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo kundi liitwalo Jukwaa la vijana wa Arewa kutoka mjini Kaduna lilitaka kampeni endelevu ya kuondoa jamii hizo kutoka Kaskazini mwa taifa hilo la Magharibi mwa Afrika