Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takribani watu milioni 41 waathiriwa na mafuriko na maporomoko Nepal, Bangladesh na India

Takribani watu milioni 41 waathiriwa na mafuriko na maporomoko Nepal, Bangladesh na India

Ofisi ya Umoja wa mataifa  ya kuratibu msaada ya kibinadamu, OCHA imesema hali ya mafuriko na maporomoko ya ardhi huko Bangladesh, Nepal na India inaweza kuwa mbaya zaidi na kuleta madhara zaidi kutokana na uwezekano wa mvua kuendelea kunyesha na maji ya mafuriko kuelekea kusini.

OCHA inasema tayari mvua kubwa imesababisha madhara ikiwemo vifo vya watu wapatao 900 kwenye nchi hizo na maelfu ya wananchi kukosa makazi,  shule na huduma za afya hospitalini.

Hata hivyo ofisi hiyo imesema serikali za nchi hizo tatu zipo mstari wa mbele kutoa huduma mbalimbali zikisaidiwa na shirika la msalaba mwekundu na hilal nyekundu, jeshi pamoja na mashirika binafsi.

Yaelezwa kuwa maeneo mengi bado hayafikiki kwa kuwa miundombinu kama vile barabara, madaraja, viwanja vya ndege na njia za reli zimeharibiwa.