UM waikosoa Marekani kushindwa kukemea siasa za ubaguzi

23 Agosti 2017

Kamati ya Umoja wa mataifa ya kupiga vita vya ubaguzi wa rangi inayoendelea na kikao chake mjini Geneva Uswis (CERD) leo  imeikosoa serikali ya marekani pamoja na viongozi wa ngazi ya juu wa kisiasa kwa kushindwa kukemea maandamano ya chuki, kibaguzi na uhalifu uliotokea Charlottesvilles Virginia na nchini kote. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Kamati hiyo ambayo inafuatilia utekelezaji wa mkataba wa kimataifa kuhusu utokemozaji wa mifumo yote ya ubaguzi wa rangi imesema “popote duniani hakupaswi kuwa na fursa ya chuki za kibaguzi na fursa ya kuruhusu fikra za utukuzaji wa watu weupe au dalili yoyote inayopinga kanuni za msingi za haki na usawa wa kibinadamu duniani kote. "

Kufuatia maandamo ya kibaguzi yaliyofanywa na makundi kama Ku Klux Klan (KKK)  na Neo Nazi yaliosababisha kifo cha Bi Heather Heyer, Mkuu wa kamati hiyo Bi Anastasia Crickley ameiomba serikali ya marekani kusimamia  sheria ya haki za kibinadamu kwa wote huku ikihakikisha inafanya uchunguzi wa kina kwa makundi hayo yenye mlengo wa kuwabagua watu wenye asili ya Kiafrica, dini  mbalimbali na haswa wahamiaji kutoka mataifa megine.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter