Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSCA yachukua hatua kudhibiti ghasia mpya Bria, CAR

MINUSCA yachukua hatua kudhibiti ghasia mpya Bria, CAR

Kufuatia kuibuka kwa ghasia mpya kwenye mji wa Bria ulioko kilometa 450 kaskazini mwa mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Bangui, Umoja wa Mataifa umeanza kuchukua hatua ili kudhibiti hali hiyo.

Ujumbe wa umoja huo nchini CAR, MINUSCA  umesema ghasia hizo ni kati ya watu wanaodaiwa kuwa masalia ya wanaopinga Balaka na kikundi cha FPRC kilichojiengua.

Hivi sasa askari na polisi wa MINUSCA wanafanya doria kwenye mji huo kuepusha watu hao kuingia mjini na hatimaye kuibua ghasia zaidi.

Halikadhalika wanalinda wakimbizi wa ndani ikiwemo wanawake na watoto kati ya 5,000 na 6,000 waliosaka hifadhi kwenye kambi ya MINUSCA.