Ukiukwaji wa sheria za kimataifa unaathari kubwa:UN women

18 Agosti 2017

Ukiukwaji wa sheria za kimataifa katika maeneo yenye mizozo umesababisha zahma kubwa ya ulinzi na uslama kimataifa. Katika ujumbe maalumu wa siku ya kimataifa ya usaizidi wa kibinadamu shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women limesema athari zake hazisemeki, mabomu na makombora yakisambaratisha shule, hospital, masoko na maeneo ya kuabudu.

Watoto wakiopolewa kwenye vifusi vya nyumba zao kila uchao huku maelfu ya wasichana wakiendelea kuwa hatarini na ndoa za mapema na shuruti na wavulana wakishinikizwa kuingia vitani na makundi yenye silaha , huku ukatili wa kingono ukizidi kusambaratisha maisha ya wanawake na wasichana.

Shirika hilo linasema katika siku hii ambayo msisitizo unatolewa kwamba raia na wahudumu wa misaada sio walengwa katika mizozo , ni lazima dunia ishikamane kubadili hali ya simanzi na madhila iliyotawala kwa raia waliojikuta katikati ya mizozo wasiyoijua chanzo chake. Limewapongeza wahudumu wa misaada ya kibinadamu kwa mchango wao mkubwa katika kunusuru Maisha ya mamilioni ya watu hao. Joselyn Sadaka mwanafunzi mkimbizi kutoka Sudan kusini miongoni mwa wanufaika wa usaidizi huo wa kibinadamu, mjini Hoima nchini Uganda

(JOSELYN CUT)

“Nashukuru Umoja wa Mataifa kwa kusaidia wajane, wenye mahitaji ya kipekee katika kambi ya Kyangwali. Bila cahkula, bila nguo, bila chochote lakini katika ushirikiano na Umoja wa Mataifa, mtu anavipata vitu hivyo. Nashukuru pia Waganda kwa kupokea na kuhifadhi na kukubali kushuriki ardhi yao ndogo na wakimbzi. Nami nafikiria kusaidia wakimbizi na Waganda kwani nami nimesiadiwa”