Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia na wafanyakazi wa misaada walindwe- Guterres

Raia na wafanyakazi wa misaada walindwe- Guterres

Wanawake ni miongoni mwa walengwa kwenye mizozo na hivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anataka walindwe. (Picha:WHD Video capture)Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya utoaji wa huduma za kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa wakazi wote ulimwenguni kulinda raia na wafanyakazi wa kibinadamu walio kwenye maeneo ya mizozo.

Msingi wa wito huo ni matukio yaliyoshamiri hivi sasa kwenye maeneo mbali mbali ya mizozo duniani ambapo mamilioni ya raia kwenye maeneo ya vita wanashambuliwa sambamba na wahudumu wanaotaka kuwaokoa.

image
Watoto nao hujikuta katikati ya mapigano na ndoto zao za kuchanua maishani huyoyoma. (Picha:WHD Video capture)
Katika ujumbe wake kwa siku hii inayobeba maudhui Si walengwa, Bwana Guterres amesema..

(Sauti ya Guterres)

“Tunataka dunia itambue raia, wakiwemo wahudumu wa misaada na wafanyakazi wa afya , sio walengwa.”

Guterres amesema raia hao wakiwemo wanawake, wanaume, wavulana, wasichana na watoto wanakumbwa na mizozo ambayo wao hawakuianzisha na hivyo kulazimika kukimbia makwao huku wakikabiliwa na sintofahamu ya mustakhbali wao, hivyo amesisitiza..

(Sauti ya Guterres)

“Tafadhali shikamana na raia kwa kupaza sauti yako kwenye kampeni yetu. Kila mtu anaweza kuleta mabadiliko katika kumaliza vurugu na kuzingatia maadili tunayoshiriki na kuyadumisha.”

Kampeni ya kulinda raia na wafanyakazi wa misaada inapatikana kwenye wavuti WWW.WorldHumanitarianDay.org