Grandi atolea wito jumuiya ya kimataifa kutambua ukarimu wa Sudan

17 Agosti 2017

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi, amefanya ziara yake ya kwanza nchini Sudan wiki hii wakati huu ambapo wakimbizi wanaendelea kukimbia mzozo nchini Sudan Kusini.

Bwana Grandi amesifu ukarimu wa watu wa Sudan, mmoja ya nchi zinazowahifadhi wakimbizi wa Sudan Kusini, na kuwa mwenyeji wa wakimbizi wengine kwa miongo akitaja kushuhudia utayari wa nchi hiyo kupokea wakimbizi miaka 30 iliyopita wakati huo akiwa afisa wa mashinani wa UNHCR.

Ameongeza kwamba wakimbizi wanapata huduma mbali mbali ikiwemo uhuru wa kufanya kazi, hata hivyo ametolea wito kwa mamlaka nchini Sudan Kusini.

(Sauti ya Grandi)

“Inahuzunisha sana kwamba mmiezi yote hii ya watu kuteseka nje ya nchi, Sudan Kusini bado haijapata amani, na hili ni jukumu la viongozi, na upinzani kuanza kuchukua hatua stahiki.”