Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Sudan Kusini walioingia Uganda sasa ni milioni 1:UNHCR

Wakimbizi wa Sudan Kusini walioingia Uganda sasa ni milioni 1:UNHCR

Idadi ya wakimbizi wa Sudan kusini waliokimbilia nchini Uganda sasa imefika milioni moja. Hii ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambalo leo limerejea kutoa ombi kwa jumuiya ya kimataifa la msaada wa haraka ili kusaidia hali ya wakimbizi hao wa sudan Kusini na serikali ya Uganda inayowahifadhi. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Katika miezi 12 iliyopita kila siku wastani wa wakimbizi 1800 wamekuwa wakiingia Uganda kutoka Sudan Kusini. Teresa Ongaro ni msemaji wa UNHCR kanda ya Afrika Mashariki, pembe ya Afrika na Maziwa makuu, anasema idadi hiyo ya wakimbizi uganda

(SAUTI YA TERESA)

Ameongeza kuwa

(SAUTI YA TERRESA2)

Tabu Sunday ni mtoto mmoja wa wakimbizi hao aliyelazimika kuwaacha wazazi wake Sudan Kusini ili kunusuru maisha yake Uganda

(SAUTI YA TABU)

Mahali nilipokuwa naishi Sudan Kusini walikuwa wanaua watu, hicho kilinifanya kukimbia Sudan Kusini. Nataka kuwa Daktari kwa sababu mtu akiumwa au mama akitaka kujifungua mtoto ninaweza kusaidia.

UNHCR inasema kwa ujumla dola milioni 883.5 zinahitajika kukidhi mahitaji ya wakimbizi wote wa Sudan kusini walioko Sudan, Kenya, Ethiopia, DRC na Jamhuri ya afrika ya Kati CAR