Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia yashikamana kukabili sumu ya zebaki kupitia mkataba wa Minamata

Dunia yashikamana kukabili sumu ya zebaki kupitia mkataba wa Minamata

Mkataba wa kwanza duniani wa kulinda afya ya binadamu na mazingira dhidi ya sumu ya zebaki umeanza kutekelezwa rasmi leo . Amina Hassan na taarifa zaidi

(TAARIFA YA AMINA)

Mkataba wa Minamata uliopigiwa upatu kwa karibu muongo mmoja, Mei 18 mwaka huu ulipata sahihi ya 50 iliyohitajika ili uanze kutekelezwa.

Mkataba huo unaziwajibisha pande 74 wadau kuhakikuisha wanapunguza hatari ya zebaki kwa binadamu na mazingira, zebaki inajulikana kuwa na athari mbaya hususani kwa watoto wachana na wale ambao bado hawajazaliwa.

Serikali ambazo ni wanachama wa mkataba huo zitawajibika kisheria kuchukua hatua mbalimbali kushughulikia athari za zebaki katika maisha yao yote. Hatua hizo ni pamoja na kupiga marufuku madini mapya ya zebaki, kutokomeza yaliyopo na kusimamia matumizi ya zebaki katika uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu, michakato ya utengenezaji na uzalishaji wa vitu vya kila siku kama vile vipodozi, balbu , betri na unga unaotumika kujaza meno.