Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna ongezeko kubwa la machafuko CAR:UNICEF

Kuna ongezeko kubwa la machafuko CAR:UNICEF

Mwaka uliopita na hususani robo ya mwisho ya mwaka huo imeshuhudia ongezeko kubwa la machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.

Donaig Le Du msemaji wa shirika hilo akizungumza leo mjini Geneva Uswis amesema CAR ni moja ya nchi ambazo ni mbaya kabisa duniani kuwa mtoto. Cha kusikitisha zaidi ameongeza ni ukweli kwamba mgogoro wa nchi hiyo unafanyika mbali na macho ya dunia na vyombo vya habari na mamilioni ya watu wa taifa hilo ndio wanaolipa gharama kubwa.

Hivi sasa inakadiriwa kwamba watu 600,000 ni wakimbizi wa ndani ikiwa ni ongezeko kubwa zaidi katika miezi mitatu iliyopita na kwamba

(DONAIG LE DU CUT)

“Mtu mmoja kati ya watano Jamhuri ya Afrika ya Kati ama ni mkimbizi nje ya nchi au ametawanywa, na hii ikimaanisha mtoto mmoja kati ya watano nchini humo hayuko nyumbani kwao au kijijini kwao . Na tuna taarifa za kutisha za ukiukwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa haki za watoto. Watoto bila shaka ni wadogo hawawezi kujilinda kijiji kinaposhambuliwa na hivyo ndiyo tunapata ukiukwaji.”

Hadi mwisho wa Jualai ombi la msaada wa kibinadamu la UNICEF la dola milioni 46.3 kwa ajili ya watoto CAR lilikuwa limefadhiliwa kwa asilimi 42 tu. Ombi hilo ambalo liliongezwa na kufikia zaidi ya dola milioni 58 sasa lina pengo la asilimia 63.