Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtoto aliyenyonyeshwa ana uhusiano mzuri na jamii-Sehemu ya tatu

Mtoto aliyenyonyeshwa ana uhusiano mzuri na jamii-Sehemu ya tatu

Wiki ya unyonyeshaji duniani imehitimishwa juma hili, kuchagiza unyonyeshaji katika miezi sita ya kwanza ya mtoto ili kumrutibisha, kumjenga kiafya na kumuepusha na maradhi yanayoweza kusababisha kifo kama Pepopunda au Pneumonia na ukuaji bora.  Katika sehemu ya tatu ya makala hii Amina Hassan anaendelea kuzungumza na Tuzie Edwin, Afisa Lishe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini Tanzania ambaye leo kufafanua manufaa ya kunyonyesha mtoto kwa mama.