Manusura na maiti zaidi wapatikana pwani ya Yemen:IOM

Manusura na maiti zaidi wapatikana pwani ya Yemen:IOM

Katika siku tatu zilizopita wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM wamewapata manusura lakini pia maiti zaidi kufuatia zahma ya boti wiki iliyopita.

Tarehe 9 na 10 Agosti jumla ya wahamiaji 280 walikuwa wakielekea nchi za Ghuba walipotoswa baharini kutoka kwenye boti mbili Pwani ya Yemen jimbo la Shabwa na wasafirishaji haramu wa binadamu.

Maiti 29 wakiwemo Waethiopia wanaume 12, wanawake 12 na Wasomali wanaume watano zilizpatikana na idadi ya watu ambao hawajulikani walipo sasa ni sita.

Maiti zingine 12 za Waethiopia wanane wanaume na wanawake wanne zilipatikana tarehe 10. Na watu 18 wanahisiwa kufa maji. Kwa mujibu wa IOm katika mkasa huo wa boti mbili jumla ya watu 53 wanahisiwa kufa maji na 18 hawajulikani walipo.