Somalia yasherehekea miaka 3 bila polio, WHO yatoa tahadhari

14 Agosti 2017

[caption id="attachment_324666" align="aligncenter" width="615"]hapanapalepoliosomalia

Mjini Mogadishu kumefanyika tukio maaluma la kusherehekea miaka mitatu tangu kisa cha polio kugundulika nchini Somalia.

Akizungumza katika tukio hilo lilohudhuriwa na wawakilishi kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Shirika la afya ulimwenguni, WHO na wizara ya afya ya Somalia, mkurugenzi wa kanda ya Mashariki mwa Mediterenea, WHO Dr Mahmoud Fikri amepongeza nchi ya Somalia kwa juhudi zake katika kukabiliana na ugonjwa huo hatarishi lakini akawahimiza kuendelea kwa na juhudi za kuudhibiti.

Ameongeza kuwa ukosefu wa visa vipya vya polio nchini Somalia ni ishara ya uongozi, dhamira na juhudi za serikali na watu wa Somalia na msaada kutoka kwa wadau.

Aidha ameongeza kuwa ni muhimu kuzingatia kwamba Somalia iko katika hatari ya maambukizi mapya na ni lazima kuchukua tahadhari.

Ukosefu wa usalama na kutofikiwa kwa baadhi ya maeneo ni baadhi ya changamoto nchini Somalia zinazokwamisha juhudi za kuwafikia watoto walio na umri chini ya miaka mitano na chanjo lakini njia bunifu zimesaidia katika kukabiliana na tatizo hilo.

Mlipuko wa polio uliozuka miaka mitatu iliyopita katika pembe ya Afrika uliwaathiri watoto mia mbili, huku Somalia ikikabiliwa na takriban asilimia 90 ya visa hivyo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter