Visa vya kipindupindu yemen vyafika 500,000:WHO

14 Agosti 2017

[caption id="attachment_323473" align="alignleft" width="625"]hapanapalewhoyemen

Idadi ya visa vinavyoshukiwa kuwa ni kipindupindu nchini Yemen mwaka huu vimegonga nusu milioni, na watu takribani 2000 wamepoteza maisha tangu kuanza kusambaa wa ugonjkwa huo mwishoni mwa mwezi April.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO kwa ujumla visa vimepungua nchi nzima tangu mapema Julai hususani katika maeneo yaliyoathirika zaidi , lakini visa vipya vimeendelea kujitokeza nchi nzima na kuambuziza watu takribani 5000 kwa siku.

Mlipuko wa kipindupindu Yemen ambao ndio mkubwa zaidi kwa hivi sasa duniani umesambaa haraka kutokana na kuzorota kwa hali ya usafi na kusambaratika kwa mfumo wa maji nchini humo, ambapo mamilioni ya watu hawana huduma ya maji safi na ukusanyaji wa maji taka umesita katika miji mingi mikubwa.

WHO inasema mfumo wa afya unaoporomoka nchini humo hauwezi kukabiliana na hali hiyo, wakati vituo zaidi ya nusu vya afya vikiwa vimefungwa kutokana na uharibifu, kusambaratishwa au ukosefu wa fedha.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter