Hali Yazidi kuwa tete Gaza mgao wa umeme ukiendelea:UM

11 Agosti 2017

Maelfu ya watu Gaza wako katika hali tete wakati huu mgao wa umeme ukiendelea na hali ya maisha kuzidi kuwa mbaya. Hii ni kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ambayo imeitaka Israel, mamlaka ya Palestina na Gaza kuzingatia haki za binadamu za watu katika eneo hilo.

Msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ni Ravina Shamdasani

(RAVINA SHAMDASANI CUT)

“Tumeshuhudia hali ikizidi kuwa mbaya kwa wanaume, wanawake na watoto Gaza. Tumewaona watoto wakiongolea kwenye maji machafu ili kupata afueni ya joto kali, familia ambazo zinapata mgao wa umeme kwa saa chache saa tisa alfajiri, na hiyo inasababisha kuvuruga usingizi kwa kila mtu, ni hali ya kukarahisha.”

Katika taarifa yake ofisi ya haki za binadamu imesema vikwazo vya Israel dhidi ya Gaza vinaendelea kuathiri raia na ni lazima viondolewe. Imeongeza kuwa hatua za kukata umeme, kupunguza mishahara na kulazimisha wafanyakazi wa umma kustaafu mapema zina athari za moja kwa moja kwa haki za watu wa Gaza katika masuala ya kijamii na kiuchumi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter