Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WaSyria 600,000 warejea nyumbani miezi 7 ya mwanzo 2017:IOM

WaSyria 600,000 warejea nyumbani miezi 7 ya mwanzo 2017:IOM

Kati ya Januari za Julai mwaka huu , Wasyria zaidi ya laki sita waliotawanywa na machafuko wamerejea nyumbani kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na wadau wengine.

Takwimu zinaonyesha kwamba wengi wa watu wanaorejea takribani asilimi 84 walikuwa ni wakimbizi wa ndani Syria, huku asilimia 16 wanarejea kutoka Uturuki , wakifuatiwa na Lebanon, Jordan na Iraq.

Wakimbizi wanaorejea kutoka Uturuki na Jordan IOM inasema wanarudi katika majimbo ya Aleppo na Al Hasakeh. Inakadiriwa kuwa asilimia 27 ya wanaorejea wanasema wanafanya hivyo ili kulinda rasilimali zao au nyumba zao, na wengine asilimia 25 wanasema ni kwa sababu hali ya uchumi imeimarika. Olivia Headon ni msemaji wa IOM..

(OLIVIA CUT)

“Ukiangalia sababu ambazo wamezitoa watu wanaorejea utaona kwamba watu wengi wanahofia mali zao, watu wengi wanahisi wamechukua hifadhi ambako hali ya uchumi sio nzuri na hawawezi kuhudumia familia zao, wanafikiri kurejea nyumbani inaweza kusaidia, unaona kwamba watu hawakuweza kuchangamana katika maeneo walikokuwa wakihifadhiwa kwa sababu ya tofauti za mahusiano ya kikabila.”