Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa Amua wahitimisha awamu ya kwanza: UNFPA Tanzania

Mradi wa Amua wahitimisha awamu ya kwanza: UNFPA Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA nchini Tanzania limekamilisha ukusanyaji wa mawazo bunifu kutoka kwa vijana yahusuyo afya ya uzazi kupitia mradi uitwao Amua ambao umedumu kwa miezi sita.

Mradi huo umehitimisha awamu ya kwanza ya uibuaji wa mawazo ambapo baada ya kupokea mawazo zaidi ya 300, mawazo ya makundi manne yameibuka washindi na hivyo UNFPA kwa kushirikiana na wadau itayawezesha mawazo hayo kuwa miradi ya kutatua changamoto za afya ya uzazi.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii Robert Ngalomba ambaye ni Mtalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano ( ICT) wa UNFPA Tanzania, amesema kile ambacho wamejifunza katika mchakato huo.

( Sauti Ngalomba)