Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji kutoka Afrika Magharibi wakabiliwa na madhila makubwa:IOM

Wahamiaji kutoka Afrika Magharibi wakabiliwa na madhila makubwa:IOM

Shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji IOM leo imetoa ripoti mpya inayoainisha madhila yanayowakabili wahamiaji kutoka nchi za Afrika ya Magharibi wanaojaribu kwenda kusaka Maisha bora ughaibuni.

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na ofisi ya IOM Niger imefadhiliwa na Muungano wa Ulaya na inatokana na maelezo ya hiyari ya wahamiaji 6000 waliosaidiwa na IOM katika vituo sita nchini Niger 2016, lakini pia uchambuzi wa kituo cha kimataifa cha takwimu za wahamiaji kilichopo Berlin Ujerumani.

Ripoti hiyo inaonyesha kuenea kwa taarifa zisizosahihi au kutopata taarifa za nini kinachowasubitri wahamiaji hao wakiwa safarini, na hali ya maisha watakayokabiliana nayo katika nchi wanakokwenda hususani Libya.

Asilimia 60 ya wahamiaji ambao sasa wanaishi Libya au Algeria wameelezea kukabiliwa na unyanyasaji mkubwa na hata kugeuzwa watum