Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutawajumuisha vijana kwa maslahi yao:Guterres

Tutawajumuisha vijana kwa maslahi yao:Guterres

Wakati siku ya kimataifa ya vijana ikiwadhimishwa kote dunia Agosti 12, Umoja wa Mataifa umesema umejizatiti kuliwezesha kundi hilo na kulijumuisha kote duniani.

Katika ujumbe wake wa video kuhusu siku hiyo, Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres amesema katika kuhakikisha azma hiyo inatimia amamteua mwakilishi maalamu mpya wa vijana Jayathma Wickramanayake ambaye ni mjumbe mdogo kabisa katika timu yake na akaongeza.

( Sauti Guterres)

‘‘Pamoja tunaweza kujenga dunia yenye amani kwa vizazi vijavyo.’’

Kwa upande wake mteule huyo wa hivi karibuni anayewakilisha vijana Bi Wickramanayake amesema licha ya wingi wa vijana duniani hadi kufikia bilioni 1.8 kiwango ambacho amesema ni kikubwa kabisa katika historia, kundi hilo linakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo ajira.

( Sauti Wickramanayake)

‘‘Leo hii, vijana milioni 73 hawana ajira. Zaidi ya vijana milioni 600 wanaishi katika hali tete au katika mazingira yaliyoathiriwa na vita. Na zaidi ya vijana milioni 400 hawana fursa ya huduma muhimu za afya.’’

Mwakilishi huyo wa vijana ameongeza kuwa katika kukabiliana na changamoto hizo mkakati wao ni..

( Sauti Wickramanayake)

 ‘‘Tumejizatiti kufanya nao kazi kwa bidi na kwa ajili ya vijana kutambua na kudimisha haki zao, na kuchagiza uraia wao wa kimataifa. Na hilo ndilo niko hapa kulifanya.’’