Stahamala muhimu kuhakikisha ulinzi kwa wakimbizi: Shearer

10 Agosti 2017

Stahamala ni mbinu bora ya kuwalinda raia katika kwa kambi za wakimbizi dhidi ya uvamizi wa kijeshi, nchini Sudan Kusini, amesema mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS, David Shearer.

Kiongozi huyo alikuwa akizungumza mjini Bentiu, Kaskazini mwa Sudan Kusini, ambapo raia zaidi ya 115,000 wanaishi katika kituo cha ulinzi wa raia cha UNMISS, kituo ambacho ni kikubwa zaidi kati ya vile vilivyo chini ya ujumbe huo.

Bwana Shearer amesema licha ya upungufu wa rasiliamali, UNMISS ina jukuma la kuhakikisha ulinzi kwa watu hao lakini akasema ..

( Sauti Shearer)

‘‘Hapa kuna maeneo ambayo watu waweza kwenda na kuanza maisha yao upya, kuna maeneo ambayo twaweza kuyafikia ambayowatu hujisikia salama. Tunachojaribu kufanya ni kuwahamasisha watu waende katika maeneo hayo ambapo waweza kuotesha mazao yao wenyewe ili wajiondoe katika utegemezi wa kuwa kambini. Hilo linatutarajia sisi kuweka vikosi vya kuhakikisha usalama kwa watu hao kuweza kurejea huko.’’

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter