Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanasanyansi DRC wazuia mlipuko wa mafua ya avian kwa kutumia nyuklia

Wanasanyansi DRC wazuia mlipuko wa mafua ya avian kwa kutumia nyuklia

Wanasayansi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wamebaini mlipuko mpya wa mafua ya ndege aina ya avian kwa kutumia teknolojia ya nyuklia . Na kwa kubaini haraka na mapema mlipuko wa virusi hivyo kumesaidia kuchukua hatua za haraka na sasa mlipuko huo umedhibitiwa na kusalia tu katika jimbo la ziwa albert karibu na mpaka wa Uganda wamesema wanasayansi hao.

Hii ni mara ya kwanza kubainika kwa mafua hayo ya ndege aina ya H5N8 nchini DRC. Kwa mujibu wa Curé Georges Tshilenge Mbuyi mkuu wa maabara ya Kati mjini Kinshasa walishangazwa lakini walikuwa na bahati ya kubaini mlipuko huo mapema na hivyo kuweza kuudhibiti.

Akiongeza kuwa kuzuia kusambaa kwa mlipuko huo ni muhimu sio tu kutokana na athari zake kwa ndege kama kuku , lakini pia yanaweza kuambukizwa kwa binadamu.

Tshilenge Mbuyi na timu yake wamejifunza jinsi ya kubaini virusi na kutafsiri matokeo katika mafunzo ya karibuni yaliyoandaliwa na shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA na shirika la chakula na kilimo FAO.