Naibu mwakilishi wa UM Somalia ajadili usalama na viongozi

9 Agosti 2017

Naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Raisedon Zenenga leo amekuwa na mazungumzo na uongozi wa jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia kujadili hatua zilizopigwa na serikali katika sekta ya usalama.

Ziara ya bwana Zenenga pia ilijikita katika ujenzi unaoendelea kwa makao makuu ya jeshi la Taifa la Somalia kikosi cha 60 na chuo cha mafunzo ya kijeshi ambao umekuwa ukifadhiliwa na serikali ya Uingereza.

Ameongeza kuwa kuwepo kwake huko ni kutathimini hatua zilizopigwa kwa ushirika na Umoja wa Mataifa, wahisani wa kimataifa , washirika wa kimataifa wanaofanyakazi na Umoja wa Mataifa, na jimbo la kusini Magharibi ili kusaidia miradi mbalimbali ikiwemo ya usalama.

Makao makuu na chuo hicho cha mafunzo vikikamilika vitahifadi maafisa wa kijeshi na pia kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama ili kuviimarisha wakati vikijiandaa kuchukua jukumu la usalama wa taifa kutoka kwa vikosi vya Muungano wa Afrika nchini humo AMISOM.

Katika majadiliano yao wamekubaliana kuendelea kutoa msaada wa kijeshi na kibinadamu kwewnye jimbo hilo ili kulisaidia kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii zinazolikabili hivi sasa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter