Mtoto aliyenyonyeshwa ana uhusiano mzuri na jamii-Sehemu ya Kwanza

8 Agosti 2017

Wiki ya unyonyeshaji duniani huadhimishwa na Umoja wa Mataifa kila mwaka kuanzia Agosti 1-7, ili kuchagiza unyonyeshaji katika miezi sita ya kwanza ya mtoto kumrutibisha, kumjenga kiafya na kumuepusha na maradhi yanayoweza kusababisha kifo kama Pepopunda au Pneumonia na ukuaji bora. Katika makala hii Amina Hassan amemhoji Tuzie Edwin, Afisa Lishe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini Tanzania ambaye anaanza kwa kufafanua umuhimu wa unyonyeshaji kwa mtoto.