Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau Mauritania tatueni tofauti kwa njia ya amani:Guterres

Wadau Mauritania tatueni tofauti kwa njia ya amani:Guterres

[caption id="attachment_324267" align="aligncenter" width="614"]barazamauritania

Kufuatia kura ya maoni ya katiba iliyofanyika Agosti 5 mwaka huu katika Jamhuri ya Kiislam ya Mautitania, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewachagiza wadau wote kuhakikisha wanatatua tofauti zao kwa njia ya amani , kwa kuzingatia sheria na kuheshimu haki za uhuru wa kukusanyika na kujieleza.

Kufuatia taarifa iliyotolewa na msemaji wake leo, Guterres ametoa wito kwa raia wote wa Mauritania kushirikiana kwa pamoja kupanua wigo wa utawala wa sheria, kuchagiza mshikamano wa kijamii na umoja wa kitaifa.