Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya waandishi wawili wa Iraq

UNESCO yalaani mauaji ya waandishi wawili wa Iraq

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, leo amelaani vikali mauaji ya waandishi wawili wa habari nchini Iraq. Ripota Harb Hazaa al-Dulaimi na mpiga picha Soudad al-Douri, maiti zao zilikutwa katika kijiji cha Imam Gharbi Kusini mwa Mosul Julai 20 .

Bi Bokova amesema vifo vyao ni kumbusho baya la gharama zinazolipwa na wafanyakazi jasiri wa vyombo vya habari waliojitolea kuhakikisha jamii inahabarishwa. Ameongeza kuwa kuwalenga waandishi wa habari katika maeneo yenye mizozo ni uhalifu wa kivita usiokubalika kwa mujibu wa mikataba ya Geneva.

Waandishi wote wawili wamearifiwa kuuawa Julai 7 wakati wakiripoti kuhusu vita vinavyoendelea kwa ajili ya televisheni ya Iraq ya Hona Salaheddinon.