Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa haki za wanawake kufuatiliwa Samoa: UM

Ulinzi wa haki za wanawake kufuatiliwa Samoa: UM

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, watafanya zaira ya siku kumi kuanzia tarehe 8 mwezi huu nchini Samoa, kwa ajili ya kubaini hatua zilizopigwa na serikali katika kupambana na ubaguzi dhidi ya wanawake, kuhakikisha ulinzi na kuinua haki zao.

Kamala Chandrakirana, Mtaalamu wa haki za binadamu ambaye kwa sasa anaongoza kikundi shupavu cha Umoja wa Matifa kuhusu ubaguzi dhidi ya wanawake kisheria na kivitendo amesema, wanalenga kubaini jinsi mabadiliko ya kisheria na sera yaliyofanywa miaka ya hivi karibuni yameathiri hali ya haki za binadamu.

Mtaalamu huyo ameongezea kuwa wataangazia nyanja mabalimbali za maisha ya wanawake ikiwemo ushiriki kisiasa na kijamii, kiuchmi, kitamaduni, maisha ya familia na usalama wao.

Wakiwa ziarani Samoa, watalamu hao watakutana na mafisa wa serikali, wawakilishi wa tasisi za serikali na asasi za kiraia, wanazuoni na wanawake binafsi.

Kikundi hicho kitawasilisha ripoti kuhusu ziara ya Samoa kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi Juni 2018.