Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko kabla ya kura ya maoni Mauritania yatia hofu:UM

Machafuko kabla ya kura ya maoni Mauritania yatia hofu:UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema inatiwa wasiwasi na machafuko yaliyojitokeza kabla ya kura ya maoni ya katiba iliyopangwa kufanyika Jumamosi ya wiki hii nchini Mauritania. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Ofisi hiyo inasema kibubwa ni ukandamizaji wa wale wanaopaza sauti zao na ripoti za matumizi ya nguvu kupita kiasi ynayofanywa na serikali dhidi ya viongozi wa maandamano.

Maandamano yamekuwa yakifanyika kila siku tangu Julai 21 yakiongozwa na wanasiasa wa upinzani wakitoa wito wa watu kugomea kura hiyo.

Serikali imearifiwa kutojibu maombi ya kuruhusu maamndamano kufanyika yna imekuwa ikitawanya waandamanaji huku viongozi wa maandamano hayo wakitripotiwa kupigwa na wengine kukamatwa. Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SHAMDASAN CUT)

“tunaitaka serikali kuhakikisha kwamba hatua dhidi ya maandamano zinakwenda sanjari na wajibu wake chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu, na kuhakikisha kwamba haki ya kukusanyika kwa amani, uhuru wa maoni na kujieleza hizi haki ni za msingi sana kabla ya uchaguzi.”