Bei ya chakula yapanda kwa mwezi wa watu mfululizo:FAO

3 Agosti 2017

Bei ya chakula duniani imepanda kwa mwezi wa tatu mfululizo mwezi Julai ikisukumwa zaidi na nafaka, sukari na bidhaa za maziwa.

Kwa mujibu wa orodha ya bei ya vyakula inayotolewa na shirika la chakula na kilimo FAO mwezi Julai bei imeongezeka kwa pointi 179.1 ikiwa ndio ongezeko kubwa kabisa tangu mwezi Januari 2015, na ni ongezeko la point 2.3 ikilinganishwa na mwezi juni.

Bei ya nafaka imepanda kwa pointi 5.1 Julai huku bidhaa za maziwa zikiongeza point 3.6. na sukari pointi 5.2.

Hata hivyo FAO inasema bidhaa kama mafuta ya kupikia bei imeshuka na nyama bei kusalia palepale.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter