Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Polisi wanawake wana mchango mkubwa kwenye UM:Appelblom

Polisi wanawake wana mchango mkubwa kwenye UM:Appelblom

Polisi wanawake wana mchango mkubwa katika miakakati ya ulinzi na usalama ya Umoja wa Mataifa hasa kwenye maeneo mbalimbali duniani waliko na operesheni za ulinzi wa amani.

Kauli hiyo imetolewa na Bi Maria Appelblom mkuu wa kitengo cha polisi wa akiba cha Umoja wa Mataifa akizungumza na UN News amesema ..

(MARIA CUT 1)

“Katika mazingira mengi tunayofanya kazi maafisa wa polisi wa kike huitajika kwa ajili ya wanawake wengi kuzungumaa nao endapo kuna mwanamke aliyebakwa na sio rahisi kuongea na afisa mwanaume na pia katika baadhi ya tamaduni ni vigumu kwa ujumla mwanamke kuzungumza na mwanaume.”

Ameongeza kuwa pia ni muhimu kuwa na maafisa wa polisi wanawake kama mfano wa kuigwa kwenye Umoja wa Mataifa lakini kikubwa zaidi ni mchango wao katika jamii..

(MARIA CUT 2)

“Nadhani ni muhimu sana tuzungumzie wanawake kama wanaharakati, wanawake kama mawakala wa mabadiliko, tunatambua kutokana na utafiti kwamba kujumuisha wanawake katika michakato ya amani inasaidia kuwa na amani endelevu, hili ni eneo ambalo nadhani tunapaswa kujikita zaidi.”