Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumeshuhudia madhila ya Boko haramu kwa watu:IOM

Tumeshuhudia madhila ya Boko haramu kwa watu:IOM

Tumeshuhudia madhila kwa watu yalkiyosababishwa na uasi wa Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing baada ya kuzuru eneo hilo.

Karibu watu milioni mbili wamezikimbia nyumba zao sababu ya Boko Haram, huku zaidi ya nusu ya watu waliotawanywa na uasi huo ni watoto na wengine 133,000 ni watoto wachanga.

Bwana Swing ametumia siku tatu katika eneo hilo akikutana na wakimbizi wa ndani kwenye makambi na katika jamii zilizoathirika vibaya hasa jimbo la Borno ambalo ndio kitovu cha machafuko ya Boko Haram kwa mwaka wa nane sasa.

Balozi Swing amekuwa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria tangu tarehe 28 Julai kushuhudia hali halisi na jinsi ya kuwasaidia maeldfu ya watu wanaohitaji msaada