Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya watoto Zanzibar imenitendea haki

Mahakama ya watoto Zanzibar imenitendea haki

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika ulinzi wa watoto baada ya kufungua mahakama mpya kwa ajili ya ulinzi wa watoto. Mahakama hiyo ni ya tatu kufunguliwa Zanzibar na hutumika kusikiliza na kutoa hukumu za kesi kati ya familia na mtoto, mtoto mtukutu, mtoto na mtu mzima na kesi zingine za watoto wenye umri wa chini ya miaka 18.

Katika makala hii Amina Hassan amezungumza na mmoja wa wanufaika Bi Rikizi Hamadi Kirango kutoka Dongembiji kisiwani humo na hapa anaanza kwa kueleza jinsi alivyonufaika na mahakama hii.