Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kisiwa cha Tonga chafanikiwa kutokomeza matende:WHO

Kisiwa cha Tonga chafanikiwa kutokomeza matende:WHO

Ufalme wa Tonga , kisiwa katika bahari ya Pacific ni kidogo na idadi ya watu wake ni wachache lakini kinafanikiwa kutimiza malengo makubwa ya kiafya umesema leo Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, limethibitisha kwamba nchi hiyo imetokomeza ugonjwa wa matende kama tatizo la afya ya umma. Matende ni ugonjwa unaoambukizwa na mbu na uathiri mishipa na kusababisha kuharibu maumbile hasa ya miguu, maumivu na ulemavu.

WHO inasema kwa watu walioathirika na matende, mabadiliko ya mauambile na unyanyapaa ni tatizo kubwa, na mara nyingi watu hupoteza uwezo wao wa kuishi, kuathirika kisaikolojia mfano kupata msongo wa mawazo na huzuni ya muda mrefu.