Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asilimia 80 ya vijana watumia intaneti: ITU

Asilimia 80 ya vijana watumia intaneti: ITU

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la muungano wa habari na Tekinologia ya mawasiliano (ITU), inaonyesha kuwa idadi ya vijana wanaotumia mtandao wa intaneti inazidi kuongezeka, wakisalia na mchango wa asilimia kubwa zaidi ya watumiaji wa mtandao huo kote duniani, huku wanaotumia Mobile Broadbadn wakitarajiwa kufikia bilioni 4.3. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Ripoti hiyo itwayo ‘ICT ukweli na takwimu 2017, imebaini kuwa vijana milioni 830 wanaotumia mtandao wa intaneti katika nchi 104 ni sawa na asilimia 80 ya vijana katika nchi hizo.

Pia imeonyesha kuwa vijana wa umri kati ya miaka 15-24 ndio wako msitari wa mbele kukumbatia matumizi ya intaneti hasa katika nchi zinazoendelea ambako wanachangia asilimia 35 huku katika nchi zilizoendelea ikiwa ni asilimia 13.

Hatimaye matumizi ya Mobile Boradmband yameripotiwa kupanda kwa asilimia 20 kawa mwaka katika miaka mitano iliopita.

Viunganishi vya kidigitali vinachangia kiasi kikubwa kwa ustawi wa jamiii kupitia ufunguzi wa nafasi za kupata maarifa, ajira na kipato kwa mabilioni ya watu kote duniani, amesema Katibu Mkuu wa ITU, Houlin Zhao.