Vita dhidi ya ubaguzi wa rangi lazima vifanikiwe:UM

31 Julai 2017

Vita dhidi ya mifumo yote ya ubaguzi wa rangi ni lazima vifanikishwe kwani mamilioni ya watu wanapitia mifumo mbalimbali ya ubaguzi wa rangi duniani pasi sababu yoyote. Grace Kaneiya na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA GRACE)

Kauli hiyo imetolewa na Adam Andemoula mkurugenzi wa kitengo cha baraza na mifumo ya mikataba kwenye ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi, katika mwanzo wa kikao cha 93 cha kamati ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi.

Amesema watu wengi wanakabiliwa na ubaguzi wa rangi wa kimfumo na kitaasisi mfano katika masuala ya haki, elimu, afya, ajira au hata makazi. Kana kwamba hiyo haitoshi, Bwana Andemoula ameongeza kuwa mamilioni ya watu pia kote duniani wanakabiliwa na ubaguzi wa rangi kupitia hotuba za chuki na uhalifu , na jamii sasa inaonekana kuwa tishio badala ya chombo cha mshikamano.

(Sauti ya Adam)

"Hakika tunaishi katika wakati mgumu ambapo ubaguzi wa rangi unarejeshwa na kuhalalishwa kwa jina la usalama na utaifa".

Kikao hicho cha 93 kitaendelea hadi Agosti 25.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter