Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajenda ya 2030 inafahamika, lakini kuifanikisha ndio mtihani: Hongbo

Ajenda ya 2030 inafahamika, lakini kuifanikisha ndio mtihani: Hongbo

Ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu inajadiliwa vyema kote duniani , lakini bado ni safari ndefu katika kuifanikisha.

Huo ni mtazamo wa Msaidizi wa Katibu Mkuu katika Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii, DESA, anayeondoka madarakani bwana Wu Hongbo.

Leo ikiwa siku yake ya mwisho katika wadhifa huo amesema malengo hayo 17 yaliyoafikiwa na nchi zaidi ya 190 takribani miaka miwili iliyopita yanapewa kipaumbele na nchi nyingi ambazo tayari zimeshawalisha tathimini yao kwa hiyari.

Miongoni mwa malengo hayo ni kutokomeza umasikini, njaa na kutoa elimu bora kwa wote. Bwana Hongbo anasema hapo ndio mtihani..

(CUT HONGBO-1)

‘Changamoto ni kwamba bado tuko mbali katika kutimiza malengo haya, hilo ni tatizo, kwa mfano lengo namba moja, kutokomeza umasikini uliokithiri katika mifumo yote, bado tuna karibu watu milioni 800 wanaishi katika umasikini uliokithiri.”

Sasa nini kifanyike?..

(HONGBO CUT 2)

“Kwanza ni uelewa wa kisiasa wa umuhimu wa kufikia malengo haya ya SDG’s, uzalishaji na matumizi yetu kwa sasa sio endelevu, huu ni msingi ambao nchi wanachama 193 walikubaliana kwa mafanikio.”