Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu mpya wa UNSMIL kuisaidia Libya kutoka kwenye sokomoko

Mkuu mpya wa UNSMIL kuisaidia Libya kutoka kwenye sokomoko

Kazi ya kuisaidia Libya kujikwamua kutoka kwenye sokomoko la kisiasa ndio kipaumbele cha kwanza cha mkuu mpya mteule wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL.

Mwanadiplomasia mkongwe kutoka Lebanon na mwanazuoni Ghassan Salamé amekuwa hapa makao Makuu ya umoja wa Mataifa New York kuzungumza na maafisa wa Umoja wa Mataifa na mabalozi kabla ya kuelekea Libya wiki hii.

Alikuwa Paris Ufaransa kwa ajili ya kutia saini azimio na viongozi wawili wa kisiasa , jambo ambalo limekaribishwa na baraza la usalama.

Bwana Salamé akizungumz a na UN news amesema tangu uteuzi wake ulipotangazwa mwezi Juni amekuwa akipokea barua pepe nyingi na ujumbe wa twitter kutoka kwa watu wa Libya

(SAUTI YA SALAME)

“Ninashukuru kwa ujumbe niliosoma mmoja unasema kama ni wewe maana yake ni kwamba mgogoro utatatuliwa hivi karibuni, au kama ni wewe tunafahamu kwamba tumepata mtu ambaye kwa hakika atasilikiza sauti zetu, nimeguswa sana na hili.”

Na kuhusu umuhimu wa mikutano yake na mabalozi kwenye Umoja wa Mataifa amesema

(SAUTI YA SALAME2)

“Kwa sababu nitakuwa na mtazamo halisi wa jinsi Libya inavyoangaliwa kwanza na nchi 5 wajumbe wa kudumu lakini pia na nchi zingine ambazo zina maslahi ya moja kwa moja na mabadiliko ya Libya na mashirika ya kimataifa kama EU na Muungano wa Afrika.”