Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bloga wa Vietnam aachiliwe baada ya mapungufu katika kesi:UM

Bloga wa Vietnam aachiliwe baada ya mapungufu katika kesi:UM

Kufungwa kwa mmiliki wa blog kwenye mtandao nchini Vietnam mwezi mmoja baada ya mwanaharakati mwingine wa mtandaoni ajulikanaye kama Mother Mushroom kuwekwa kizuizini ni ishara ya kuongezeka kwa msako dhidi ya watetezi wa haki za binadamu umeonya leo Umoja wa Mataifa.

Onyo hilo lililotolewa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa limekuja baada ya Tran Thi Nga kuhukumiwa miaka tisa jela na miaka mitano ya kifungo cha nyumbani kwa kile kinachosemerkana kufanya propaganda za kupinga serikali mtandaoni. Kesi yake ilidumu kwa siku moja kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Liz Throssell, ambaye amesema Tran alikwekwa katika mahabusu ya kutengwa kwa miezi sita kabla ya kufikishwa mbele ya jaji.

Ofisi hiyo imeongeza kwamba katika miezi sita iliyopita takribani watetezi wengine saba wa haki za binadamu wamekamatwa na kukabiliwa na mashitaka, na wengine wengi wako mahabusu huku wawili wamesafirishwa kwa nguvu au kupelekwa ukimbizini nje ya nchi . Watetezi wengine wanatishwa, kunyanyaswa na kupata kipigo.

Ofisi ya haki za binadamu imetoa wito wa kuachiliwa kwa watetezi wote wa haki walioko kizuizini na kufanyia marekebisho sheria za kuwasaka watetezi hao kwa kisingizo cha usalama wa taifa.