Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutaimba na kucheza ngoma hadi amani irejee Darfur

Tutaimba na kucheza ngoma hadi amani irejee Darfur

Mapigano baina ya vikundi vya waasi na serikali vya muda mrefu sasa yamepungua kutokana na jitihada za wadau wa kimataifa kusaidia nchi hiyo kurejesha tena amani. Baada ya miongo na miongo ya mateso na madhila ya vita hivyo, nuru ya amani inaangazia jimbo hilo na katika makala ifuatayo Amina Hassan anakupeleka huko kuangazia jinsi watu wa Darfur wameamua kutoa ngoma zao nje, kuimba na kucheza kwa ajili ya amani kama ilivyokuwa desturi yao hapo awali. Ungana naye.