Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vanuatu kutumia drones kufikisha chanjo vijijini:UNICEF

Vanuatu kutumia drones kufikisha chanjo vijijini:UNICEF

Serikali ya Vanuatu imesema itaaanza majaribio ya kutumia ndege zisizo na rubani au drones kufikisha chanjo za kuokoa maisha katika jamii za vijijini kwenye kisiwa hicho.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limethibitisha taarifa hizo leo na kusema ndege hizo zisizo na rubani zitajaribiwa kwa mara ya kwanza katika kisiwa hicho cha Pacific.

Shirika hilo limeongeza kuwa lengo ni kupima uwezo, ubora na utendaji wa ndege hizo zisizona rubani katika kufikia maeneo ya ndanindani vijijini na maeneo yasiyofikika.

Kwa mujibu wa UNICEF awamu ya kwanza ya majaribio hayo itafanyika Agosti 21 hadi 25 mwaka huu.