Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres akaribisha kutatuliwa mvutano Jerusalem

Guterres akaribisha kutatuliwa mvutano Jerusalem

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha habari za kutatuliwa kwa mvutano kwenye mji wa kale wa Jerusalem kwa kuzingatia hadhi ya maeneo matakatifu iliyowekwa kabla ya Julai 14.

Kupitia taarifa ya msemaji wake , Katibu Mkuu amesema anatumai kwamba majadiliano yataendelea na kuchangia kuweka mazingira ya uaminifu miongoni mwa jamii katika eneo hilo.

Ameongeza kuwa Katibu mkuu ataendelea kujihusisha na wadau wote katika suala hili.