Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yatoa muongozo mpya kuzisaidia nchi kufuatilia maliasili ya misitu

FAO yatoa muongozo mpya kuzisaidia nchi kufuatilia maliasili ya misitu

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limetoa muongozo mpya wenye lengo la kuzisaidia nchi kuanzisha mfumo imara wa kitaifa ambao ni muhimu katika kupima hatua zilizopigwa kwenye mchakato wa kutimza malengo ya maendeleo endelevu, SDG’s katika suala la misitu.

Kwa mujibu wa FAO ili kutimiza ahadi zao chini ya mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris na ajenda ya maendeleo ya 2030, nchi zinatarajiwa kukusanya takwimu zaidi kuhusu misitu yao.

Takwimu hizo hazitojumuisha tu taarifa za ukubwa na ukuaji au kupungua kwa misitu. lakini pia masuala muhimu ya kuhakikisha misitu endelevu kama vile jukumu la misitu katika uhifadhi wa bayoanuai, kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kutoa huduma zingine katika mfumo wa maisha.

FAO inasema taarifa kuhusu misitu katika nyanja ya kijamii na kiuchumi, ikijumuisha mchango wa misitu katika maisha ya watu na kupunguza umasikini, imekuwa suala muhimu katika mipango ya kitaifa.

Muongozo huo mpya utasaidia sana katika mipango, kubadilishana uzoefu, na utekelezaji katika suala zima la udhibiti wa misitu.