Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Uganda wakiwezeshwa ,wanajiweza

Vijana Uganda wakiwezeshwa ,wanajiweza

Kama zilizovyo nchi nyingi barani Afrika tatizo la ajira kwa vijana Uganda limekuwa donda ndugu, na fikra za kumaliza masomo na kuajiriwa zimesalia kuwa hadhithi za abunuwasi. Sasa vijana hao wametambua ili kujikimu sio lazima wategemee kuajiriwa bali kujiajiri kwa njia mbalimbali. Na hilo sio tu litawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuinua pato la taifa bali litasaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira na kubweteka. Mwandishi wetu John Kibego alipata fursa ya kukutana na baadhi ya vijana na kuzungumza nao , ungana naye katika makala hii.