Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania tumefanikiwa katika ukaguzi wa hesabu za serikali-Profesa Assad

Tanzania tumefanikiwa katika ukaguzi wa hesabu za serikali-Profesa Assad

Tanzania imepiga hatua kubwa na kupata mafanikio katika zoezi la ukaguzi wa hesabu za serikali. Kauli hiyo imetolewa na Profesa Mussa Assad mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali wa Tanzania aliyeko hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhuduria mkutano unaotathimini ukaguzi wa hesabu za serikali na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s. Profesa Assad anaanza kwa kutaja mafanikio.