Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulengaji wa makusudi wa raia katika mashambulizi ni ukiukaji wa haki:Guterres

Ulengaji wa makusudi wa raia katika mashambulizi ni ukiukaji wa haki:Guterres

Ulengaji wa makusudi wa raia katika mashambulizi ni ukiukaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa ambao unahesabiwa kama uhalifu wa kivita.

Hayo yamo katika taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kulaani vikali shambulio la kigaidi la kujitoa muhanga lililotokea leo nchini Afghanistan.

Katika taarifa hiyo iliyowasilishwa na msemaji wake, Antonio Guterres amesema kundi la kigaidi la Taliban limedai kuhusika na uhalifu huo.

Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waathirika na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi.

Amerejelea kusisitiza mshikamano wa Umoja wa Mataifa na watu na serikali ya Afghanistan katika wakati huu mgumu na katika vita dhidi ya ugaidi.