Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhusiano mzuri kati ya Eritrea na UM, ni faida kwa wananchi

Uhusiano mzuri kati ya Eritrea na UM, ni faida kwa wananchi

Mkataba wa miaka mitano kuanzia mwaka huu wa 2017 hadi 2021 kati ya Umoja wa Mataifa na uongozi wa Eritrea unalenga kuimarisha hali ya kibindamu nchini humo.

Akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Mkuu wa operesheni katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA John Ging amesema hii ni ishara ya mabadiliko ya uhusiano kati ya nchi hiyo na Umoja wa Mataifa ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka 2012 wakati Umoja huo ulikuwa na wazo la kuondoka nchini humo ambako serikali ya Eritrea ilikuwa hawaridhishwi na jumuiya ya kimataifa na jumuiya ya kimataifa vile vile na hiyo wananachi ndio waliumia.

Bwana Ging ameongeza kuwa licha ya uhasama huo lakini Umoja wa Mataifa haukukataa tamaa..

(Sauti ya Ging)

“Viongozi wenye subira wa Umoja wa Mataifa walianza kuangazia maswala ambayo wangekubaliana nayo kama shirika na tukalenga mambo muhimu tunayoyafanya na matokeo ya kazi zetu kwa watu wa Eritrea, serikali ilitambua hilo na hatua kwa hatua tukajenga uwelewano na hivyo kuanza ushrikiano wa miaka minne kati ya 2013-2016 na matokeo mazuri ya ushirkiano huo yamechangia kuingia mkataba wa miaka mingine mitano.”

Mkuu huyo amesema tofauti na mpango wa awali uliojikita katika maswala ya huduma ya afya hususan kwa watoto na wanawake, elimu na kilimo katika nchi hiyo inayokabiliwa na hali ya ukame mara kwa mara lakini..

(Sauti ya Ging)

“Cha ziada katika mkataba huu mpya ni kwamba kuna miradi kuhusu maswala ya kijinsia, haki za bindamu, vijana na uhamiaji, hizi ni changamoto kubwa kwa Eritrea na hiyo inaonyesha ushirikiano mzuri ambao upo katika mamlaka ya Eritrea na ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo.”